51Թ

Zaidi ya watu 250,000 wakimbia machafuko yanayoendelea Ituri -UNICEF

Get monthly
e-newsletter

Zaidi ya watu 250,000 wakimbia machafuko yanayoendelea Ituri -UNICEF

UN News
21 May 2020
By: 
 Wakimbizi wa Burundi katika makazi ya Mulongwe huko Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.
UNHCR/Georgina Goodwin
Wakimbizi wa Burundi katika makazi ya Mulongwe huko Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Watu zaidi ya robo milioni wengi wakiwa ni watoto wamekimbia machafuko yanayoendelea kushika kasi katika jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC tangu mwanzoni mwa mwaka huu limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF.

Shirika hilo linasema huku ni kuongeza shinikizo kwa huduma za kibinadamu ambazo tayari zimeathirika katika jimbo hilo lililo moja ya majimbo masikini kabisa, yasiyo na usalama na lililoghubikwa na maradhi nchini DRC.

Taarifa hiyo yainasema watu 200,000 walikimbia katika maeneo ya Djungu, Mahagi na Irumu na kupata hifadhi katika jamii, na makazi ya wakimbizi wa ndani ambayo yamefurika kupindukia tangu mwishoni mwa mwaka jana kwenye eneo la Bunia mji mkuu wa jimbo la Ituri .

Adha zinazowakabili wakimbizi

Imeongeza kuwa hali katika eneo la Djungu ni mbaya zaidi hasa ukizingatia kwamba asilimia 70 ya wahudumu wa kibinadamu ilibidi wasitishe operesheni zao kutokana na kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama.

Takribani wakimbizi wapya wa ndani 25,000 ambao walikwenda kwenye makambi sasa wanahaha ku[ata fursa ya maji salama na usafi.

Hata kabla ya wimbi jipya la wakimbizi, watu waliotawanywa walikuwa wanaweza kupata lita tano tu za maji kwa siku ikiwa ni kiwango kidogo sana chini ya kiwango cha wastani kinachopendekezwa kwa siku.

Athari za machafuko yanayoendelea

Kuendelea kwa machafuko UNICEF inasema kumesababishwa kuharibiwa kwa vituo 22 vya afya katika jimbo la Ituri, kuibiwa kwa akiba kubwa ya chanjo na vifaa vya baridi vya kuhifadhi madawa. Pia shule Zaidi ya 160 zimeharibiwa au kuporwa.

Ukosefu wa malazi, lishe, huduma za afya na elimu kumewaacha Watoto katika hatari kubwa ya ukatili, machafuko na kunyanyaswa imesema taarifa hiyo ya UNICEF.

Na kuongeza kuwa kati ya Aprili na Mei pekee UNICEF imepokea madai Zaidi ya 100 ya ukiukwaji mkubwa wa haki za Watoto ikiwemo ubakaji, mauaji, kujeruhiwa, mashambulizi dhidi ya shule na vituo vya afya.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa UNICEF nchini DRC Edouard Beigbeder,“Hali jimboni Ituri inazorota kwa haraka, tunahitaji kuchukua hatua haraka iwezekanavyo ili kuepusha mgogoro ambao utalazimisha watoto zaidi.”kukimbia na kuwaweka hatarini.”

Juhudi za UNICEF nchini DRC

Shirika la UNICEF limeendelea kuhakikisha uwepo wake nchini DRC na kuendesha operesheni za kuokoa Maisha hasa jimboni Ituri kupitia utekelezaji na wadau mbalimbali, lakini limesema mahitaji ya watu ni makubwa na yanaendelea kuongezeka.

Maelfu ya Watoto wako katika hatari ya utapiamlo uliokithiri, Maelfu kwa maefu wengine hawahudhurii shule na huenda wasi na madarasa ambako wanaweza kwenda kusoma shule zitakapofunguliwa.

Na magonjwa hatari kama suria yanaendelea kylighubika jimbo hilo.

Sasa ombi la hatua za kibinadamu lakwa ajili ya kuwasaidia Watoto nchini DRC n idola milioni 262. Na hadi kufikia tarehe 15 Mei n idola milioni 5.5 tu ndizo zilizopokelewa na dol zingine milioni 28.8 zilichukuliwa kutoka zile za mwaka jana na hivyo bado kuna pengo kubwa la ufadhili la doola milioni 229 sawa na asilimia 87 ya fedha zinazohitajika.